Kila lenye mwisho basi lilikuwa na
mwanzo wake, na dalili ya mvua ni mawingu ingawaje baadhi ya wakati
inaweza kunyesha bila ya hata kuonekana mawingu, kwenye upande wa
mapenzi zipo dalili za kuachwa au kuachika.1.Mwenza
kukosa raha mnapokuwa pamoja, mara nyingi unapokuwa nae karibu anakosa
furaha na hii ni kutokana na kutokuhitaji uwe nae karibu.
2.Kutopenda kutembelewa ikiwa mnakaa
sehemu tofauti au kukutaka utowe taarifa kabla ya kumtembelea, kama
ulikuwa una tabia ya kwenda kwake bila kumtaharifu, maisha yatabadilika
na kuhitaji taarifa kabla ya kwenda kumuona.
3. Kutoipa umuhimu mitoko yenu kama
ilivyokuwa awali, mara nyingi hatokuwa akihitaji kuwa karibu na wewe na
mitoko ya awali haitokuwepo na hatakuwa ahishiwi visingizio kila ukitaka
mtoke.
4. Kuanzisha majibu ya mkato, tofauti
na awali ataanza kukujibu majibu yasiyokupendeza wakati mwingine anaweza
akaa kimya kabisa bila kukujibu au akakujibu kwa mkato.5.Kutozijibu meseji zako kwa wakati tofauti na ilivyokuwa awali,
mawasiliano yenu yatapungua kwa asilimia kubwa na hii sio kwa meseji tu
wakati mwingine hata kupokea simu inaweza ikawa ni tatizo.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment