Mnamo 18 May, ushindi wa Sevilla mbele ya Liverpool jijini Basel uliwapa nafasi ya tano ya kushiriki kwenye Super Cup – mara zote wakiwa mabingwa watetezi wa UEFA Cup/UEFA Europa League. Siku 10 baadae, Real Madrid wakawafunga mahasimu Atlético Madrid kwa penati na sasa wanaelekea Norway kwenye Super Cup wakiwa na matumaini ya kurudia ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Sevilla mnamo 2014 katika UEFA Super Cup jijini Cardiff. Lakini siku 5 kabla ya mchezo huo, Real Madrid wana changamoto tano zinazompasua kichwa kocha wao Zinedine Zidane….
1. Hakuna No. 9
Magoli
matatu aliyonayo Marcelo yanamfanya awe mfungaji bora wa Madrid katika
michezo ya pre season inayoendelea, lakini jambo hili linatia shaka
ukizingatia majeruhi ya Benzema wakati Morata bado hajafiti vizuri
kwenye timu. Zidane atakuwa bila mshambuliaji yoyote kutoka kwenye
kundi la BBC katika mchezo wa fainali vs Sevilla na tayari amegundua
Morata bado hajafiti kwenye mfumo wa timu. Mchezaji wa kikosi cha
Castilla, Mariano anaweza kutumika baada ya kucheza vyema na kufunga
katika mchezo vs Chelsea.
No. 2: Wachezaji wasiojua hatma yao kikosini
No. 3: Kutokuwepo kwa Kroos na Modric
Huku
wakiwa na pengo la Kroos na Modric katika safu ya kiungo, Isco na
Kovacic walionyesha kiwango kibovu katika michezo ya kirafiki, lakini
hili haliwezi kusemwa kwa Marco Asesnio, kijana wa miaka 20, amekuwa
mmoja wa wachezaji bora wa Madrid katika pre season. Kabla ya ziara ya
pre season, hatma yake ndani ya klabu ilikuwa haieleweki lakini
kuelekea mchezo wa Super Cup, kinda huyu aliyezaliwa eneo la Mallorca
amemshawishi Zidane na huenda akaanza, lakini bado kukosekana kwa
Modric na Kroos ni changamoto nyingine inayomuumiza kichwa Zizzou.
4: Muda mfupi wa kuandaa mfumo wa 442.
Mara
tu ilipo fahamika kwamba Cristiano Ronaldo hatocheza mchezo wa Super
Cup jijini Trondheim, Zidane alianza kufanya maandalizi ya kutumia
mfumo wa 4-4-2 kwa matumaini ya kuwatumia Morata na Benzema kwenye
ushambuliaji. Majeruhi ya Benzema yamempa changamoto Zizzou ya upangaji
wa kikosi huku kukiwa hakuna member hata mmoja wa BBC katika mchezo
huo.
5: Maandalizi yasiyotosheleza ya Pre Season
Real
Madrid watakuwa wamecheza mechi 3 tu mpaka kufikia mchezo wao vs
Sevilla, hivyo bado damu zao zitakuwa hazijakaa sawa na hili
lilionekana wazi katika mchezo dhidi ya PSG ambao ndani ya dakika 30 za
mwanzo, Madrid alikuwa kashapigwa 3 kwa makosa ya wachezaji ambao
walionekana miili yao haikuwa na utayari. Backline ya
Marcelo-Varane-Nacho-Carvajal haikuonekana pia kuwa vyema katika mchezo
vs Chelsea.
0 comments:
Post a Comment