NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

LEMA- VIONGOZI WA DINI MSHAURINI JPM,LABDA ATAWASIKIA

 

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, wamewaomba maaskofu na mashehe kusaidia kumshauri Rais John Magufuli akubali kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

Walisema endapo viongozi hao wa dini, watafanikiwa katika ushawishi wao, nchi itaepuka uwezekano wa kuingia kwenye machafuko kutokana na utekelezaji wa Operesheni Ukuta waliyotangaza kuanza Septemba Mosi mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Chadema wa Kanda ya Kaskazini, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbless Lema, alisema ni viongozi wa dini pekee ndio wanaweza kusaidia kumshauri Rais Magufuli ili vyama vya siasa, viruhusiwe kufanya mikutano ya hadhara.

Alisema msimamo wa wabunge wa Chadema wa Kanda ya Kaskazini ni kufanya mikutano kuanzia Septemba Mosi ili kudai uhuru wa vyama vya siasa wa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano, kama njia ya kukuza demokrasia nchini.

“Wakati bado tunasuguana sisi na vyombo vya dola, tunawaomba viongozi wetu wa dini maaskofu, mashehe na wachungaji wamshauri Rais wetu ili atuachie uhuru huu ambao ni wa kikatiba ,” alisema Lema.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment