Ni vizuri utambue kuwa
unapoamua kufanya tendo la ndoa ni vyema ukajua mahitaji ya mwenzio iwe
mwanaume/mwanamke, jaribu kumfanyia mwenza wako vitu vya tofauti na
alivyovizoea ama ambayo anatarajia kuviona kwako kutokana na mazoea.
Ukifanya hivyo utamfanya aendelee kuwa na hamu ya kuwa na wewe kwa muda
mrefu.
Naweza kusema mwacheni Mungu
aitwe Mungu. Mara nyingi mtoto anapozaliwa kuna baadhi ya vitu huwa
anafundishwa lakini baadhi ya vitu huwa havihitaji kufundishwa. Kwa
mfano hakuna mtu anayemfundisha mtoto kulia, kunyonya, kujisaidia,
kucheka, kulala.
Japo kuna baadhi ya vitu
ambavyo pindi akikua atatakiwa kuachana navyo na kufanya vya kiutu uzima
kama suala la kujisaidia. Kwa sababu yeye hujisaidia ndani ya nguo yake
ama popote pale, hivyo hufika muda akaelekezwa jinsi ya kujisaidia
kuliko salama. Ndivyo hivyo na katika ndoa.
Hakuna mtu aliyewahi
kufundishwa jinsi ya kufanya tendo la ndoa. Wewe hapo ni shahidi, lakini
kuna baadhi ya vitu hulazimishwa kufundishwa kulingana na mazingira
husika. Ndiyo maana kuna baadhi ya makabila kuwafunda watoto wao kabla
ya kuingia katika masuala ya ndoa.
Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kukusaidia katika kuifanya ndoa yako iwe imara ya yenye furaha wakati wote;
A. Uwe mbunifu wa kuangalia ni sehemu ipi ukimshika mke/mumeo anasisimka.
B. Ujue mwili wako na wa mpenzi wako kwa kila mmoja wapi aguswe ili asikie raha.
C. Mweleze mwenzako sehemu ambazo unapenda awe anazichezea ili akupe hisia zaidi.
D. Jiamini katika kutafuta mitindo ambayo itakuwa faida kwa ndoa yenu.
E. Kila mmoja awe wazi kwa mwenzake na ushirikiano wa mpenzi yenu uwe mzuri.
F. Ujue sehemu za kumsisimua kwa utundu na ufundi wako mwenyewe.
G. Muulize sehemu anazopata msisimko ili uzifanye naye asike raha wakati wa faragha.
H. Yajue yanayomkosesha raha ya kufurahia tendo la ndoa.
I . Yajue mambo yanayomletea hisia haraka za kufanya mapenzi.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment