Mara nyingi asilimia kubwa ya wanawake hupenda kuwa na wanaume
wanaojiweza kiuchumi. Lakini baadae wanapotambua kwamba mwanaume huyo
ameshaoa hushangaa sana, huumia na kusema waliwaamini kuwa wako single
na kwamba wanaume wote ni mbwa tu.
Wanaume sio mbwa au paka shume, ni nyie wenyewe ndio mnashindwa
kuwaelewa na hamtaki kufanya uchunguzi. Mlishaambiwa kwamba nyuma ya
mwanaume mwenye MALI na MAFANIKIO kuna mwanamke. Na wewe unataka
mwanaume aliyefanikiwa. Unategemea nini?
Kama utakutana na mwanaume ambae ni handsome, ana mali, anaendesha gari
nzuri, yuko vizuri kiuchumi, basi huyo sio mumeo mtarajiwa, huyo ni mume
wa mtu fulani kwa muda huo. Ni agharabu sana kukutana na mwanaume
anayejiweza halafu akawa single, either uwe shareholder au unyang'anye
share zote za mwanamke mwenzako kitu ambacho sio busara hata kidogo.
Mume wako mtarajiwa yupo anahangaika kutoka na maisha, anapigania ndoto
zake. Huenda yupo shambani, yupo dukani, anapiga kitabu chuo, au yupo
anabeti. Kimsingi yupo anapigania kuchomoka kimaisha. Anakusubiri tu
wewe umpe support na back up ya kutosha.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment